Nakuruto alihisi mavune mwili mzima. Uchovu aliohisi ulikuwa sawa na mtu aliyeburura rukwama kutwa nzima. Aliufungua mlango wa chumba chake cha kulala, taratibu akajikokota hadi kitandani. Alijitupa huko kama gunia la viazi. Muda si muda, aliingia katika ulimwengu wa ndoto. Alijitenga na uhalisi uliomzunguka, uhalisi uliomkera kwa siku nyingi na kumpa majonzi yasiyokwisha, uhalisi wa ajabu uliokiuka uhalisi wa kawaida. Naam, ulikuwa uhalisi uliomchacharisha, ukamtia kiwewe na chachawizo la moyo. Hii ndiyo maana alipotupia jicho kitanda tu, alihisi kupata afueni kwani mahali hapo pangemsahaulisha masumbufu yaliyomsibu, ingawa kwa muda. Ama kweli, alimshukuru Muumba kwa kuwaumbia waja usingizi kwani dunia ingejaa wehu ikiwa watu wangepokonywa hali hii tulivu.

Weitere Produkte vom selben Autor

No Edges Momanyi, Clara, Mtanga, Fadhy, Shafii, Fatma, Israel, Lusajo Mwaikenda, Mahugu, Mwas

16,00 €*
Kidole cha Habiba Momanyi, Clara

12,50 €*
No Edges Israel, Lusajo Mwaikenda, Kezilahabi, Euphrase, Mahugu, Mwas, Mkangi, Katama G C, Momanyi, Clara, Mtanga, Fadhy, Shafii, Fatma, Mbaga, Lilian

18,50 €*
Siku ya Wajinga Momanyi, Clara

16,90 €*